Header Ads

MAMBO MATANO UTAKAYOMFANYIA MKEO/MMEO/MCHUMBA UNAEMPENDA KWELI AMBAYO AWALI ULIYAONA YA ‘KIPUUZI’

Unapokuwa unampenda mumeo/Mkeo/Mchumba wako kweli hasa ambaye mmeanza uhusiano wenu siku za karibuni, kuna tabia ambazo utaanza kuonesha ‘automatically’ ambazo huenda zamani uliziona ni upuuzi. Hapa utakuwa unasukumwa na mapenzi ya moyo na utakuwa unapenda kufanya mara kwa mara kama sehemu ya vitu unavyovipenda sana.

1. Kumuangalia machoni kwa umakini mara kwa mara
Kumuangalia Machoni mara kwa mara, hasa unapotaka kumwambia kitu muhimu kama ‘nakupenda sana’, au kumuahidi kitu, kumuaga kama unasafari n.k. utajikuta unamuangalia muda mrefu machoni. Na wengine humshika kabisa kichwani au mikono yote miwili na kumuangaia kwa muda mrefu huku wakitoa maelezo mafupi mafupi kueleza kiasi gani anampenda.

2. Ubishani wa vitu vidogo sana unaoimarisha mapenzi
Bila shaka ulishawahi kusikia wachumba au wanandoa (hasa ikiwa bado haijachukua muda mrefu) wakibishana hata kwa muda mrefu kuhusu nani anampenda mwenzake zaidi, au wakati wanaiongea na simu wakibishana nani aanze kukata simu, ‘kata wewe’.

Unaweza kuuona kama upuuzi fulani hivi lakini kama hujaoa au hujapata mchumba, ukiingia katika maisha hayo hasa mwanzoni utajikuta unapenda kufanya hivyo. Ni njia nzuri pia inayodumisha na kuimarisha uhusiano lakini unaweza kuiona kama ni mchezo tu.

3. Kutumia sahani moja/kijiko kimoja wakati wa kula
Unaweza kuwa kwa kawaida umezoea kula chakula kwa kupakua na kutumia sahani yako na wenzako pia kufanya hivyo.
Lakini unapokuwa umezama kwenye mapenzi na mwanandani wako/ mahabuba utajikuta unapenda kula nae chakula kwa kutumia sahani moja na hata kutumia kijiko kimoja. Hapo ndio utaona raha ya kulishana hata kama awali ulikuwa unaona wanaofanya hivyo wanafanya ‘utoto’.

4. Kumuita majina mazuri ya mapenzi hasa kutafuta litakalokuwa lako pekee
Katika mapenzi kuna kitu kinaitwa ‘ubunifu’, hapa lazima utajikuta umekuwa ‘msanii’ wa aina yake. Utaliondoa jina halisi la mpenzi wako na kuanza kumuita majina matamu mara kwa mara ‘baby’, ‘sweetie’, ‘mahabuba’ n.k. Haya yamezoeleka. Lakini kwa wabunifu zaidi hutafuta majina yao wenyewe kwa wapenzi wao kama ‘pumziko’ au hata majina ya kilugha ambayo yana maana nzuri sana ya kitu fulani cha thamani sana.

5. Kuoga pamoja na kufanya nae kazi ambazo wengi wangeziita ‘za kike/kiume ‘
Mahaba yanapokolea, moja kwa moja ile formula ya 50/50 inaweza kuanza kuonekana kwa mbali bila kulazimishwa. Utajikuta unapenda sana kufanya nae kazi kadiri uwezavyo kwa kuwa unapenda muda mwingi uwe karibu nae. Hapo utajikuta unapenda kupika nae chakula, kumsaidia kufua au kusuuza nguo n.k.

Lakini kitu ambacho huenda ulikuwa unakichukulia poa ni pale unapoona wanandoa wanasubiriana na kuingia bafuni pamoja. Ukizama kwenye mapenzi utajikuta unapenda sana kuona na mwenzi wako. Ratiba yenu utajitahidi iwakutanishe bafuni muoge na kutaniana.

Kwa Ushauri wa Kisaikolojia na Mahusiano, Wasiliana na Amani Missanah Kupitia Namba : 0658027027

No comments