Header Ads

Timu ya kwanza kushuka daraja VPL

Timu ya JKT Ruvu imekuwa ya kwanza kushuka daraja katika msimu huu wa ligi kuu Tanzania bara mara baada ya kupoteza mechi yake ya ugenini kwa kipigo cha bao 2-1 dhidi ya Toto Africans ya Mwanza.
Magoli ya Waziri Junior aiyefunga magoli yote yameizamisha JKT Ruvu na kuirudisha ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Goli pekee la JKT Ruvu limefungwa na Hassan Dilunga ambalo halikuwasaidia kitu katika mchezo wa leo wakiwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
JKT Ruvu ina pointi 23 baada ya kucheza mechi 28 ikiwa imebakiza mechi mbili pekee kabla ya msimu kumalizika. Hata kama watashinda mechi zao mbili zilizosalia kwenye ligi, watafikisha pointi 29 ambazo haziwaruhusu kusalia kwenye ligi.
Msimu uliopita timu ya JKT Mgambo ilishuka daraja kwa hiyo kushuka kwa JKT Ruvu kunafanya timu mbili za jeshi la kujenga taifa kushuka daraja ndani ya misimu miwili mfululizo.
JKT Ruvu imedumu kwenye ligi kuu Tanzania bara kwa misimu 15 mfululizo baada ya kupanda daraja mwaka 2002.

No comments