Header Ads

Mbaroni kwa kukutwa na fuvu la binadamu

Mganga wa kienyeji, Moshi Mohamed Matimbwa (26), (aliyevua shati) na msaidizi wake aliyetambulika kwa jina la Ally Omari Mapande (23) wakazi wa wilayani Kibiti wamekamatwa na Polisi baada ya kukutwa na fuvu la binadamu
Akithibithisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema watu hao walikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati polisi wakiwa kwenye doria katika kijiji cha Jaribu.
Jeshi la Polisi mkoani Pwani linawashikilia watu hao wawili wakazi wa Kibiti kwa tuhuma za kukutwa na fuvu la kichwa cha binadamu.
Akithibithisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema watu hao walikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati polisi wakiwa kwenye doria katika kijiji cha Jaribu.
Lyanga amesema watuhumiwa hao waliokuwa wakitoka Mkuranga kuelekea Kibiti kwa kwa kutumia pikipiki walikuwa wameficha fuvu hilo kwenye begi.
Amesema baada ya kufika katika kijiji hicho wakiwa kwenye pikipiki walisimamishwa na polisi waliokuwa doria eneo hilo na baada kuwakagua ndipo walipokuta fuvu hilo ndani ya begi.
Amesema uchunguzi unaendelea ili kubaini mahali lilipotoka fuvu hilo.

Chanzo: Mwananchi

No comments