Header Ads

Mwakyembe Apiga Marufuku Usomaji wa Magazeti kwenye TV na Redio

Waziri Mwakyembe amesema hayo leo jijini Mwanza katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari nchini ambapo amekuwa mgeni rasmi, katika hotuba yake amezuia vyombo vya habari hasa Radio na Television kufanya uchambuzi wa kina wa magazeti bali wasome tu vichwa vya habari lengo la kuwavutia wasomaji kununua magazeti hayo kwaajili ya kupata habari kamili na kukuza biashara hiyo ya magazeti.

Mbali na hilo Mwakyembe amesema serikali itaendelea kutetea na kulinda haki za waandishi wa habari pamoja na mazingira bora ya ufanyaji kazi huku akiwahakikishia ulinzi waandishi wa habari za uchunguzi.

Mhe. Mwakyembe pia aliwasihi wanahabari kuwa wakweli na kuzingatia misingi na maadili katika kazi zao. "Mlinzi wa kwanza wa Waandishi wa Habari ni Mungu, Mlinzi wa Pili ni Kalamu ya Mwandishi mwenyewe hasa anapozingatia maadili ya kazi yake," alisisitiza Mhe. Mwakyembe.

Mhe. Mwakyembe ameilekeza Idara ya Habari ya Habari-Maelezo kuwa na utaratibu wa kukutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari mara kwa mara ili kubadilishana mawazo na kutoa taarifa sahihi za Serikali pamoja na kujadili udhaifu unaoweza kujitokeza na kuchukua hatua lengo ni kuwekana sawa

No comments