Header Ads

Mwanajeshi ajipiga picha akiuawa Afghanistan

Picha moja iliochukuliwa na mpiga picha wa jeshi nchini Marekani wakati yeye na wanajeshi wengine wanne waliuawa katika mlipuko imetolewa na jeshi la Marekani.
Mwanajeshi Hilda Clayton mwenye umri wa miaka 22 na wanajeshi wanne wa Afghanistan waliuawa wakati bomu lilipolipuka wakati wa zoezi la kijeshi mnamo tarehe 2 mwezi Juali 2013.
Jeshi la Marekani pia lilitoa picha ya mwanajeshi wa kike wa Afghanistan ambaye mtaalam Clayton alikuwa akijifunza naye kupiga picha .
Pia alifariki.
Kifo cha Clayton ni ishara kwamba wanajeshi wa kike wanazidi kukabiliwa na hatari wakati wa mafunzo pamoja na vita na wenzao wa kiume.
Ajali hiyo ilitokea katika mkoa wa mashariki wa Laghman.
Jarida la jeshi lilichapisha picha hizo.

Chanzo: BBC

No comments