Header Ads

Randers: Tunamhitaji Himid Mao kupiga kazi moja kwa moja

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Randers ya nchini Denmark, Michael Gravgaard amesema wanamhitaji kiungo mkabaji wa Azam na Taifa Stars, Himid Mao kwa ajili ya kumtumia moja kwa moja na sio kusubiri akomae kwa miaka miwili au mitatu.
Gravgaard ameeleza kuwa kwa umri wa Himid wa miaka 24 wanatarajia aoneshe kitu tofauti katika kikosi chao cha Randers.
” Himid ana angalau miaka 24, hauwezi kumzungumzua kama chipukizi. Randers tunalifahamu hili vizuri. ”
” Tumemchukua kwa lengo la kuisaidia timu moja kwa moja. Ana miaka 24, lakini hili si jambo la msingi kwa sababu kama ni mzuri basi atacheza tu bila kujali umri wake.”
” Huyu si mchezaji tunayetarajia kumkuza kwa miaka 2-3 kabla ya kuwa msaada wa kipekee kwa Randers. ”
Pia Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa wamemfuatilia Himid kwa muda mrefu na kazi hio ilifanywa kwa ukaribu na yeyeye binafsi pamoja na mkurugenzi wao wa zamani.
” Kwenye video anaonekana ni mtu wa kazi, lakini ni ngumu kutoa maamuzi kutokana na video. Kwa hio tumemualika Randers kumtazama akicheza na na watu imara zaidi. ”

Chanzo: Soka360

No comments