Header Ads

Tanzania iko pale pale viwango vya FIFA

Kwa mara nyingine Shirikisho la Soka Duniani, FIFA limetoa orodha ya viwango vya soka duniani kwa  mwezi huu.
Kwa mujibu wa viwango hivyo, Tanzania imeendelea kushikilia nafasi ya 135 Duniani kama ilivyokuwa mwezi uliopita.
Mwezi uliopita Tanzania Ilipanda kwa nafasi 26 kufuatia kushinda mechi mbili mfululizo dhidi ya Botswana na Burundi.
Tanzania haijacheza mechi yoyote tangia hapo.
Kikosi cha Taifa Stars ambacho kipo chini ya kocha mkuu, Salum Mayanga kinatarajiwa kuingia kambini mwezi huu mwishoni mara baada ya mechi ya fainali ya kombe la Shirikisho.
Kwa upande wa Afrika Mashariki, Uganda ambao ni wawakilishi pekee wa ukanda huu wameendelea kuongoza kwa kukamata nafasi ya 72,Wanafuatiwa na Kenya ( 78 ).
Hakuna mabadiliko yoyote katika nafasi 50 za kwanza duniani, huku Brazil wakiendelea kuongoza mbele ya Argentina na Ujerumani na Senegal walio katika nafasi ya 30 wakiongoza barani Afrika.

No comments