Header Ads

Umuhimu wa kutimiza majukumu katika mahusiano

Matatizo mengi leo katika mahusiano chanzo kimojawapo ni wahusika kukwepa kutimiza majukumu yao katika ndoa, tafiti zinaonyesha migogoro mingi pia huanzia katika suala zima la kutimiza majukumu na sababu mbili kubwa ni Mume kukwepa kwa makusudi kutimiza majukumu yake au kuwa na uchumi mdogo kiasi cha kushindwa kukidhi matakwa ya mahitaji muhimu ya Mkewe kama vile chakula,mavazi,malazi na matibabu.

Tukianza na hili la kwanza ambalo ndio la hatari zaidi, la Mume kuwa na uwezo lakini kwa makusudi hataki kutimiza majukumu kwa mkewe lina athari kisaikolojia na kibaiolojia
Kisaikolojia humpa mke fikra nyingi zisizo na majibu kiasi ya kupelekea mwanamke kuchanganyikiwa kwa maswali mengi atakayo kuwa akijiuliza hali ambayo inaweza kumfanya muhusika kupata maradhi ya msongo wa mawazo na hatimae kuchanganyikiwa.

Sababu kubwa atakuwa akijiuliza mara kwa mara ni vipi Mumewe hampi mahitaji yake wakati uwezo wa kufanya hivyo anao?mara nyingi majibu ya Wanawake wengi huangukia katika dhana ya kuwa pengine Mumewe ana Mwanamke mwingine nje ya ndoa yao ama kama ni ndoa ya wake wengi basi atadhani pengine Mke mwenzie anapendwa zaidi na ndie anaye patiwa mahitaji kuliko yeye na hapo ndipo chuki ya wanawake hao huanzia na kupelekea magomvi yasiyo kwisha kati yao na hata pengine kuwa na uhasama mkubwa kiasi cha kupelekea hata ndoa mojawapo kuvunjika kati yao.

Lakini athari zingine ni pamoja na Mwanamke kupoteza hamu ya kushiriki tendo la ndoa na Mumewe kwa ajili ya msongo wa mawazo, kupoteza mvuto wake kwa Mumewe kwa kukosa vifaa muhimu vinavyomfanya avutie kama vile vipodozi, mavazi chakula bora, na utulivu wa akili na uchangamfu ambao kila Binadamu anapaswa kuwa nao.

Na kibaya zaidi kwa kuwa Mwanamke huyu anahitaji mahitaji hayo muhimu ili kuhimili maisha yake kuna uwezekano mkubwa kwa Mwanamke huyo kama si Mcha Mungu basi akapata mawazo au ushauri mbaya wa marafiki wa kuwa na hawara nje ya ndoa ili kukidhi mahitaji hayo muhimu kwake kwa kisingizio cha kukopa fedha au mchezo wa kupeana maarufu kama upatu ambao hutumiwa na Wanawake wengi kujiongezea kipato kumbe kuna Buzi pembeni lina kusaidia kumtunza Mkeo jambo hili ni la hatari huongeza matatizo ndani ya ndoa na haswa ukizingatia gonjwa hatari la Ukimwi,mbali na ukimwi unaweza pia kuletewa mtoto ambaye sio wako mimba ya mchepuko na pia Mkeo akaanza kukudharau kwani tayari anapata jeuri ya huyo Mbuzi wake anae mchuna kama wasemavyo wenyewe cha hatari zaidi ufundi wa tendo la ndoa tunatofautiana sasa kama ikatokea huyo mbuzi akawa fundi zaidi kuliko wewe basi ujue safari ya kuelekea kuzimu ya ndoa yako ndio imefika.

Athari nyingine ni fedheha ya kufumaniana endapo itatokea umemfumania Mkeo na kwa kuwa hakuna siri katika mapenzi ipo siku utamfumania na athari za fumanizi ni pamoja na taarifa kuzagaa kila kona ya Dunia haswa zama hizi za mitandao ya kijamii taarifa zinakwenda kwa haraka sana mbali na taarifa hizo kuenea kuna pia kuumizana kutakako sababishwa na ugomvi au hata kifo kati yenu wagoni au uharibifu wa mali na fedheha kwa familia zenu na jamii kwa ujumla na hapa mifano ipo mingi sana kwa waliowahi kukutana na dhahma hiyo
KISAIKOLOJIA.

Pia kuna athari zake kutokana na jambo hili la Mume kushindwa kutimiza wajibu wake wa kindoa kwa Mkewe unaposhindwa kumpa mahitaji yake muhimu mkeo ikiwemo chakula bora utamsababishia kupata maradhi mbali mbali ikiwemo vidonda vya tumbo,kukosa usingizi, kupoteza hamu ya tendo la ndoa na uwezo wa kushiriki tendo hilo,lakini pia anaweza kupata matatizo ya mfumo wake wa uzazi, presha na hata kuchanganyikiwa au ugonjwa wa wasi wasi kutokana na mawazo na hatimae ukijikuta unatumia tena gharama kubwa za fedha kutafuta tiba kumbe chanzo cha tatizo hilo ni wewe mwenyewe kukwepa majukumu yako na kibaya zaidi katika matibabu unaweza kutumia gharama kubwa zaidi kuliko ambazo ungezitumia kumpa mahitaji yake mfano mwenzako anapo umwa muda ambao unautumia kumuuguza ni muda ambao ungeweza kuutumia kuingiza kipato ambacho kingewasaidia katika maisha yenu hapa unakuwa huingizi lakini pia unatoa kwa ajili ya matibabu yake kuanzia dawa,vipimo,usafiri nk.

Ikumbukwe ya kuwa kutimiza wajibu wako kama Mume katika ndoa ni jambo la lazima na sio hiari bila kujali kama kuna migogoro kuna upendo wa kweli au la ili mradi umeshafunga ndoa huna hiari kutimiza wajibu bali ni lazima ufanye hivyo na faida za kutimiza wajibu zipo nyingi sana ikiwemo heshima yako kuwa Mwanaume halisi unayejitambua na unatimiza wajibu wako uliopewa na Mola wako, inaleta upendo na utulivu ndani ya nyumba, inaondoa migogoro isiyo ya lazima, inaleta raha na heshima kwako na kwa familia nzima isipokuwa Mwanamke nay eye inabidi akubali hali halisi ya kipato cha Mumewe na mahitaji yaendane na kipato cha Mumewe sio kutaka makubwa wakati Mume hana uwezo nacho lakini pia Mume aongeze kufanya bidii katika kutafuta pato la halali huku Mkewe akimtia moyo na wote kwa pamoja mkishikirikiana kumuomba Mungu awajalie kutimiza ndoto zenu cha msingi mjiwekee malengo ya kutaka kufikia mafanikio yenu kwa uadilifu na upendo mkubwa.

Mwisho; kwa leo tafakari sana jambo hili ndugu yangu msomaji mwanaume kwani leo unao uwezo wa kumpa mahitaji mkeo na hufanyi hivyo kwa makusudi je vipi kesho wewe ukiwa huna na yeye akapata uwezo kutoka kwa Mola wake na ndio maana waungwana walinena Ilee na uitunze familia yako kwa mikono miwili wakati wa raha kwani utawahitaji sana wakati wa shida.
Credit : Amani Missanah

No comments