Header Ads

Watu watano (5) wafa kwa ajali ya basi Kaskazini mwa Msumbiji

Watu watano wamefariki dunia na wengine tisa wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea mkoani Nampula, kaskazini mwa Msumbiji.

Kwa mujibu wa Radio ya Msumbiji, basi moja la serikali lililokuwa likisafirisha wafanyakazi liligongwa na basi lingine linalomilikiwa na kampuni binafsi ya usafiri.

Hospitali kuu ya Nampula imesema, watu watatu walifariki papo hapo na wengine wawili walifariki wakiwa njiani kupelekwa hospitali hiyo.

Chanzo : CRI Kiswahili

No comments